Majukumu ya Mfuko

Majukumu
Mfuko wa Taifa wa Maji unatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Na. 5 ya mwaka 2019. Huduma zinazotolewa na Mfuko zinatokana na majukumu yaliyoainishwa katika Sheria hiyo chini ya Kifungu cha 56 [(a)–(g)] kama ifuatavyo:

  1. Kukusanya na kuhamasisha rasilimali za fedha kwa ajili ya kusaidia uwekezaji katika miradi ya maji na uhifadhi wa vyanzo vya maji;
  2. Kutoa na kupeleka fedha kwa Wakala wa Utekelezaji kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji;
  3. Kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa Wakala wa Utekelezaji kwa ajili ya uwekezaji katika miradi ya maji;
  4. Kufuatilia na kusimamia matumizi ya fedha zinazotolewa kwa Wakala wa Utekelezaji;
  5. Kujenga uwezo wa Wakala wa Utekelezaji wa miradi ya maji ili waweze kusimamia na kutekeleza miradi kwa ufanisi;
  6. Kumshauri Waziri wa Maji kuhusu miongozo ya utoaji wa mikopo kwa Mamlaka za Maji; na
  7. Kuandaa miongozo ya kiutendaji kuhusu utoaji wa mikopo na ruzuku kwa Wakala wa Utekelezaji wa miradi ya maji.

Ofisi za Mfuko wa Taifa wa Maji huwa wazi kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni. Ofisi hufungwa siku za mwisho wa wiki na siku za sikukuu za kitaifa.