Utoaji wa Ruzuku
Miradi ya maji inayostahili kufadhiliwa na Mfuko itachaguliwa kwa kuzingatia vigezo vilivyobainishwa chini ya Miongozo hii.
Kanuni ya 6 ya Kanuni za Mfuko wa Taifa wa Maji inaainisha taratibu zinazopaswa kuzingatiwa katika uteuzi wa miradi ya maji kwa ajili ya kufadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Maji. Taratibu hizi zitafuatwa kwa mujibu wa miongozo ya bajeti iliyobainishwa chini ya Sheria ya Bajeti ya mwaka 2015. Taratibu hizo zinahusisha hatua zifuatazo:—
Hatua ya 1: Utambuzi na uandaaji wa mapendekezo ya miradi na Wakala wa Utekelezaji (IAs) kwa mujibu wa Mwongozo wa Usanifu wa Sekta ya Maji unaotumika kwa wakati husika;
Hatua ya 2: Uwasilishaji wa mapendekezo ya miradi ya maji na Wakala wa Utekelezaji kwa Wizara kwa ajili ya uhakiki;
Hatua ya 3: Uwasilishaji wa orodha ya miradi ya maji kutoka Wizara kwenda kwa Mfuko kwa ajili ya tathmini na uchambuzi wa awali;
Hatua ya 4: Tathmini na uchambuzi wa awali wa orodha ya miradi iliyowasilishwa na Mfuko na utoaji wa mapendekezo kwa Waziri;
Hatua ya 5: Kuzingatia na kuidhinisha na Waziri orodha ya miradi ya maji iliyopendekezwa na Mfuko wa Taifa wa Maji;
Hatua ya 6: Kuwasilisha miradi ya maji iliyochaguliwa Bungeni kwa ajili ya kutengewa bajeti; na
Hatua ya 7: Utekelezaji wa miradi ya maji iliyoidhinishwa.