Menejimenti ya Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo yatembelea Ofisi za Mfuko wa Taifa wa Maji

30 May, 2025 - 30 Oct, 2025
10:40:00 - 14:45:00
National Water Fund Salmin – Tambukareli St Dodoma,
juma.mchiro@nwf.go.tz

Menejimenti ya Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo imetembelea Ofisi za Mfuko wa Taifa wa Maji na kupokelewa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko Bw. James Kalimanzila lengo likiwa ni kubadilishana uzoefu pamoja na kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mfuko wa Taifa wa Maji. Aidha, wataalam hao kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo waliongozwa na Bi. Maria Mtui ambaye ni Meneja wa Mfuko wa Maendeleo ya kilimo.

Menejimenti ya Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo yatembelea Ofisi za Mfuko wa Taifa wa Maji
Matangazo