Dira na Dhima
Dira na Dhima
DIRA
Kuwa chanzo cha uhakika na endelevu cha fedha za miradi katika Sekta ya Maji.
DHAMIRA
Kutafuta na kutuma fedha kwa watekelezaji wa miradi ya maji kwa ajili ya kuboresha huduma ya maji pamoja na utunzaji wa vyanzo vya maji.
MISINGI
Ili kuweza kutekeleza kikamilifu Dira na Dhamira ya Mfuko wa Taifa wa Maji watumishi wanapaswa kuzifuata Kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma pamoja na kuwa na tabia na mwenendo unaozingatia mambo yafuatayo:
- Maadili: Mfuko wa Taifa wa Maji utazingatia maadili mema katika kutoa huduma kwa Umma.
- Uwajibikaji: Mfuko wa Taifa wa Maji utahakikisha kila Mtumishi anawajibika ipasavyo katika kutimiza majukumu yake.
- Huduma bora kwa mteja: Mfuko wa Taifa wa Maji unathamini wateja wake na kutoa huduma zinazoridhisha.
- Uwazi: Mfuko wa Taifa wa Maji unathamini ufanyaji kazi kwa uwazi katika utoaji wa huduma zake.
- Ushirikiano: Mfuko wa Taifa wa Maji unazingatia ushirikiano kati ya wateja na Watumishi wake ili kufikia malengo.
- Huduma kwa matokeo chanya: Mfuko wa Taifa wa Maji unaamini katika matokeo chanya katika utoaji wa huduma kwa wateja.
Matangazo