Majukumu
Majukumu
Majukumu:
Mfuko wa Taifa wa Maji unatekeleza majukumu yake chini ya Sheria ya Usambazaji Majisafi na Usafi wa Mazingira Na. 5 ya mwaka 2019. Huduma zitolewazo na Mfuko zinatokana na majukumu yaliyoainishwa kwenye Sheria katika Kifungu cha 56 [(a) – (g)] kama ifuatavyo:
- Kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kusaidia uwekezaji kwenye miradi ya maji na utunzaji wa vyanzo vya maji;
- Kutuma fedha kwa watekelezaji kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji;
- Kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa watekelezaji kwa ajili ya kuwekeza kwenye miradi ya maji;
- Kufuatilia matumizi ya fedha zinazotumwa kwa watekelezaji;
- Kujengea uwezo watekelezaji wa miradi ya maji ili waweze kusimamia kwa ufanisi miradi inayotekelezwa;
- Kumshauri Waziri wa Maji kuhusu Miongozo ya utoaji mikopo kwa Mamlaka za Maji; na
- Kuandaa Miongozo ya kiutendaji kuhusu utoaji wa mikopo na misaada kwa Watekelezaji wa miradi ya maji.
Matangazo