Dira, Dhamira, Maadili ya Msingi

Dira

Kuwa chanzo cha kuaminika na endelevu cha ufadhili katika Sekta ya Maji.

Dhamira

Kuhamasisha na kusambaza rasilimali za kifedha kwa Taasisi za Utekelezaji kwa ufanisi ili kuboresha utoaji wa huduma za maji na kuhifadhi maeneo ya vyanzo vya maji.

Maadili ya Msingi

(i) Uadilifu

Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Maji huonesha uaminifu, maadili mema na kuzingatia misingi ya kimaadili katika utendaji wao wa kazi. Huwatendea wadau kwa uwazi na uaminifu ili kufanikisha malengo ya Mfuko.

(ii) Uwajibikaji

Mfuko utazingatia wajibu wa kukubali na kutekeleza majukumu na dhamana ulizopewa. Pia utathamini uwezo wa watumishi kutimiza wajibu wao kwa uadilifu, kuwajibika kwa matendo yao na kurekebisha makosa yanapotokea.

(iii) Uwazi

Mfuko utatekeleza shughuli zake kwa uwazi na kutoa taarifa stahiki kwa wadau wake.

(iv) Ushirikiano wa Timu

Watumishi wa Mfuko watafanya kazi kwa ushirikiano, wakitumia utaalamu, ujuzi na uwezo wao binafsi ili kufikia malengo ya Mfuko.

(v) Kuzingatia Matokeo

Mfuko utaelekeza nguvu na rasilimali zake katika kufikia malengo na matokeo yaliyokusudiwa.

(vi) Kuzingatia Mteja

Mfuko utahakikisha huduma zake zinakidhi mahitaji ya wateja kwa ufanisi na ubora, huku ukijitahidi kuzidi matarajio yao wakati wote.

(vii) Ubunifu

Mfuko utahamasisha matumizi ya mawazo mapya au yaliyoboreshwa, bidhaa, huduma na mifumo ya kazi inayoongeza thamani na kuleta matokeo yanayopimika.