Event: Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira imekoshwa na Taasisi za Wizara ya Maji kwa kazi yenye weledi.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira imekoshwa na Taasisi za Wizara ya Maji kwa kazi yenye weledi.

Taasisi hizo ni  Mfuko wa Taifa wa Maji na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), kamati ikieleza kuridhishwa na mwelekeo wa utekelezaji wa miradi ya maji inayolenga kuongeza upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama kwa wananchi. 

Kamati hiyo, ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake Mhe. Prof. Pius Yanda (Mb), imepokea na kujadili taarifa kuhusu taasisi hizo  Bungeni jijini Dodoma, zikiwasilishwa  na Wakili Haji Nandule, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Maji, na Mhandisi Wolta Kirita, Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA, kwa niaba ya Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb).  

 Kamati imesisitiza umuhimu wa kuimarisha usimamizi wa rasilimali fedha, kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi pamoja na kuhakikisha miradi inayotekelezwa inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyokubalika, ili kufanikisha malengo ya Serikali ya kuwapatia wananchi huduma ya maji endelevu na ya uhakika.