Biography & Profile
Dr. Sekela Simon Twisa ni mtaalamu wa rasilimali za maji na mazingira kutoka Tanzania, aliyezaliwa tarehe 01 Desemba 1982. Ana Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Integrated Management of Water, Soil and Waste kutoka United Nations University – Institute for Integrated Management of Material Fluxes and of Resources (UNU-FLORES) kwa ushirikiano na Technische Universität Dresden (Ujerumani). Aidha, ana Shahada ya Uzamili ya Sayansi (MSc) katika Integrated Water Resource Management kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ushirikiano na vyuo vya Botswana na Zimbabwe, pamoja na Shahada ya Kwanza ya Sayansi katika Environmental Science and Management kutoka Sokoine University of Agriculture.
Kitaaluma, Dr. Twisa amehudumu katika nafasi mbalimbali ndani ya sekta ya maji ikiwemo kuwa Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara katika Water Institute, Mratibu wa Miradi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), na Senior Environmental Officer katika Water Resources Centre of Excellence chini ya Wizara ya Maji, Dodoma.
Kwa sasa, Dr. Sekela Simon Twisa ni Mkurugenzi wa Utathimini wa Miradi na Utafutaji Rasilimali katika Mfuko wa Taifa wa Maji (National Water Fund), ambapo anasimamia tathmini ya miradi na uhamasishaji wa rasilimali kwa ajili ya maendeleo endelevu ya sekta ya maji nchini Tanzania. Ameongoza na kushiriki katika tafiti na miradi ya kimataifa inayolenga ustahimilivu wa mabadiliko ya tabianchi, usimamizi wa mabonde ya maji, pamoja na maendeleo endelevu ya rasilimali za Maji.