Nyamande T. Kazimili

Wakili Nyamande T. Kazimili

Meneja wa Kitecgo cha Sheria

Biography & Profile

Bi. Nyamande Thomas Kazimiri ni Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania na mtaalamu wa sheria mwenye uzoefu mpana katika sheria za umma na binafsi. Alizaliwa tarehe 14 Novemba 1986. Ana Shahada ya Uzamili ya Sheria (LL.M) katika Sheria ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kutoka Chuo Kikuu cha Iringa, akijikita katika masuala ya makosa ya mtandao, sheria za TEHAMA, usalama wa taarifa na biashara mtandao (e-commerce). Aidha, ana Stashahada ya Uzamili katika Mafunzo ya Uanasheria kutoka Law School of Tanzania na Shahada ya Kwanza ya Sheria (LL.B) kutoka Ruaha University College.

Kwa sasa anahudumu kama Meneja wa Kitengo cha Sheria katika Mfuko wa Taifa wa Maji, ambapo anaongoza na kuratibu masuala ya kisheria, kutoa ushauri wa kimkakati wa kisheria, na kuhakikisha uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu zinazotumika.

Kitaaluma, tangu Januari 2018, Bi. Nyamande amehudumu katika Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kama Afisa Sheria, akitoa ushauri wa kisheria, kuandaa na kupitia mikataba ya ujenzi, kuwakilisha taasisi mahakamani na katika majadiliano, pamoja na kusimamia Kitengo cha Sheria katika ngazi ya mkoa. Kabla ya hapo, alihudumu kama Afisa Sheria katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, ambapo pia aliwahi kuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria.