Biography & Profile
Scholastica Beatus Chandika ni mtaalamu wa ukaguzi wa ndani na usimamizi wa Fedha, aliyezaliwa tarehe 10 Februari 1980 mkoani Mwanza. Ana Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara (MBA – Corporate Management) na Shahada ya Kwanza ya Uhasibu na Fedha kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe. Aidha, ni Mhasibu wa Umma Aliyesajiliwa (CPA-T) chini ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA). Ana uzoefu mpana katika ukaguzi wa sekta ya umma, akifuata viwango vya Kimataifa vya Taaluma ya Ukaguzi wa Ndani (IPPF), pamoja na utaalamu katika IPSAS, usimamizi wa hatari, udhibiti wa udanganyifu na mifumo ya TEHAMA.
Kitaaluma, Bi. Chandika kwa sasa anahudumu kama Meneja wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani katika Mfuko wa Taifa wa Maji (National Water Fund) tangu Aprili 2024. Kabla ya hapo alihudumu katika Wizara ya Fedha katika nyadhifa mbalimbali kuanzia Internal Auditor II hadi Principal Internal Auditor II.