Haji M. Nandule

Wakili Haji M. Nandule

Afisa Mtendaji Mkuu

Biography & Profile

Haji M. Nandule ni Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mtaalamu Aliyethibitishwa wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP Specialist). Alizaliwa tarehe 02 Oktoba 1981 jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ana Shahada ya Uzamili ya Sheria (LLM) katika Sheria ya Biashara na Makampuni pamoja na Shahada ya Kwanza ya Sheria (LLB) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na Stashahada ya Uzamili katika Mafunzo ya Uanasheria kutoka Law School of Tanzania. Aidha, amepata mafunzo na vyeti mbalimbali vya kitaaluma ndani na nje ya nchi katika maeneo ya PPP, sheria za maji na utungaji wa sheria.

Kitaaluma, Haji Nandule amewahi kuhudumu kama State Attorney katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Senior Legal Officer katika Wizara ya Maji, na Legal Manager wa Mfuko wa Taifa wa Maji. Amehusika katika uandaaji na tafsiri ya sheria, majadiliano ya mikataba, uwakilishi mahakamani, pamoja na kuratibu kamati mbalimbali zilizosimamia uanzishwaji wa taasisi muhimu za sekta ya maji nchini.

Hivi sasa ni Afisa Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Taifa wa Maji, akiendelea kuchangia maendeleo ya sekta ya Maji na usimamizi wa Rasilimali nchini Tanzania.