Juma M. Mchiro

Bw Juma M. Mchiro

Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA na Takwimu

Biography & Profile

Juma Masoud Mchiro ni mtaalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kutoka Tanzania, aliyezaliwa tarehe 26 Aprili 1978 mkoani Morogoro. Ana Shahada ya Uzamili katika Information and Communication Technology for Development (ICT4D) kutoka College of Business Education (2019), Stashahada ya Uzamili (Postgraduate Diploma) katika Scientific Computing kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pamoja na Advanced Diploma ya Information Technology kutoka Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA). Amehudhuria mafunzo mbalimbali ya kitaaluma ndani na nje ya nchi katika maeneo ya e-Government, usalama wa mitandao, Cisco networking, LAN/WAN administration CDAC Noida, New Delhi, India, Government e-Payment Gateway (GePG), pamoja na mifumo ya udahili na usimamizi wa taarifa za vyuo vikuu.

Bw. Juma kwa sasa ni Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA na Takwimu, Mfuko wa Taifa wa Maji (National Water Fund) tangu Machi 2023. Kabla ya hapo alikuwa Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA katika Chuo cha Maji, Dar es Salaam kwa miaka kadhaa, akiongoza Maendeleo na Usimamizi wa mifumo ya TEHAMA.