Biography & Profile
Haji M. Nandule ni mtaalamu mahiri wa sheria kutoka Tanzania, Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, na Mtaalamu aliyethibitishwa (PPP) Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), mwenye uzoefu mpana katika ushauri wa kisheria wa sekta ya umma na utawala wa Taasisi. Kwa sasa ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Maji.
Ana Shahada ya Uzamili ya Sheria (LLM) katika Sheria ya Biashara na Makampuni pamoja na Shahada ya Kwanza ya Sheria (LLB – Hons) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Mazoezi ya Sheria kutoka Shule ya Sheria ya Tanzania. Aidha, amepata mafunzo maalum ya kitaaluma katika masuala ya PPP, uandishi wa sheria, pamoja na sheria za maji na mazingira kutoka taasisi mbalimbali zinazotambulika kimataifa.
Kitaaluma, Bw. Nandule amewahi kuhudumu kama Afisa Sheria Mwandamizi katika Wizara ya Maji, Wakili wa Serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na Hakimu Mkazi Msaidizi (Mafunzo). Amehusika kwa kiasi kikubwa katika uandaaji na utekelezaji wa sheria na Taasisi muhimu za sekta ya Maji, zikiwemo Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2019, RUWASA, na MDSA, na anatambulika sana kwa umahiri wake katika uandishi wa sheria, majadiliano ya mikataba, uendeshaji wa mashauri ya kisheria, na ujenzi wa uwezo ndani ya sekta ya Maji Nchini.